KAREN IGBO: ALILIA KUTONGOZWA
Mshindi mwenza wa Big Brother Afrika wa mwaka jana Karen Igbo amesema anasikitishwa na tabia ya wanaume kuogopa kumtokea akidai kuwa inaweza kumkosesha mume
Karen anasema wanaume wanamuogopa kutokana na jina lake anasisitiza kuwa sio kigezo cha wao kushindwa kurusha ndoano zao kwani mwisho wa siku anahitaji kupendwa
"Mimi ni mwanamke tena ninahitaji sana kutokewa kwani wakati mwingine huwezi jua na mimi nimekupenda lakini kutokana na mila zetu za kiafrika siwezi kukutokea" anasema Karen