Google PlusRSS FeedEmail

KHADIJA KOPA KUKUTANA NA TWANGA PEPETA




Bendi ya muziki wa dansi ya The African Stars 'Twanga Pepeta'leo usiku ataungana na 'Malkia wa Mipasho' Khadija Kopa kutoa burudani katika Ukumbi wa Mzarendo Pub Millennium Kijitonyama Dar es Salaam

Licha ya burudani hiyo ya taarabu na muziki wa dansi pia kutaporomoshwa muziki wa mayenu na madj bora nchini Dj Mackay na Dj Too Short

Akizungumza jijini Dar es Salaam Ofisa Habari wa kampuni ya Mac D Promotions, Peter Mwendapole ambaye ndiye anayeratibu onesho hilo, maandalizi yote yamekamilika kilichobaki ni muda ufikie watu wapate burudani

"Kila kitu kipo sawa siku hiyo watu watakaofika watashuhudia burudani bila kikomo kwani Twanga Pepeta wamejiandaa vyema kuangusha shoo ya nguvu ikiwa ni pamoja na kuwakumbusha mashabiki wake enzi za shika ungo upepete na kisigino

"Na malkia wa mipasho Bi. Khadija Kopa atazipiga nyimbo zake zote za zama na zile za sasa hivyo mashabiki wa burudani wanatakiwa kufika kujionea wenyewe " alisema

Alisema kiingilio katika burudani hizo ambazo zitakuwa tatu kwa mpigo kitakuwa sh. 10,000 na mashabiki wataselebuka hadi asubuhi

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging