MASHUJAA KUVAMIA KIGAMBONI
Bendi ya muziki wa dansi Mashujaa 'Wanakibega' kwa mara ya kwanza kesho watafanya onesho lao maalum Kigamboni katika ukumbi wa Mamaz and Papaz
Akizungumza Dar es Salaam Meneja wa bendi hiyo Martin Sospeter alisema ni mara ya kwanza kwa bendi hiyo kufanya onesho Kigamboni
Alisema wapenzi wa kigamboni watarajie burudani nzuri kutoka kwa rais huyo watapata nafasi ya kuona staili mpya ya kibega kwa wanenguaji wa bendi hiyo pamoja na nyimbo zao mpya kama vile Risasi kidole na Usidharau Sufuri