Mshindi atakayeibuka kidedea katika mashindano ya kumtafuta mfalme wa hip pop yaliyopewa jina la 'Mkali wa Mic'anatarajiwa kuzawadiwa gari pamoja na kuinuliwa kimuziki
Akizungumza Dar es Salaam jana mratibu wa mashindano hayo Abdallah Mrisho ambaye pia ni Meneja wa Matukio wa Dar Live, alisema mashindano hayo yataanza jumapili wiki hii katika uwanja wa burudani wa Dar Live
Alisema washiriki wa mashindano hayo ni vijana ambao hawajatoka kimuziki, ila ni katika aina ya muziki wa kufokafoka ambao watashindana na majaji mbalimbali watawachuja na baadaye kupatikana mshindi
Mrisho alisema zawadi ya mshindi katika mashindano hayo ni gari, ambalo litatambulishwa hivi karibuni ambapo pia mshindi atapata nafasi ya kuendelezwa kimuziki ikiwa ni pamoja na kutayarishiwa albamu yake