VAZI LA SUTI HUONESHA UNADHIFU WAKO
Leo tena katika safu hii ya Urembo tutaangalia vazi la suti kwa wanawake , vazi hili mara nyingi humfanya mvaaji aonekane nadhifu na mwenye heshima kubwa ndani ya jamii anayoishi
Mrembo ambaye pia alishawahi kushiriki mashindano mbalimbali ya urembo Jacqueline Cliff yeye alizungumzia vazi lla suti kuwa ni vazi la heshima na linakufanya wanajamii wakuangalie kwa jicho la umakini zaidi Alisema kuwa vazi la suti ni vazi linalopendwa na wanawake pamoja wanaume hivyo alisema kuwa anapenda kuongelea vazi la suti kwa upande wa wanawake zaidi
Mara nyingi vazi la suti ni vazi la kuheshimika hivyo aliongezea kuwa vazi hilo huvaliwa zaidi kanisani, kazini, kwenye sherehe na mikutano mbalimbali
Alielezea aina ya suti kuwa zipo za aina nyingi zipo za mikono mifupi, na zile za mikono mirefu, pia kuna suti za vipande vitatu na za vipande viwili na ili upendeze zaidi wengine wanaweka skafu ambayo ina rangi za kufanana na suti au kofia
Ili suti ionekane vizuri na uonekane mtanashati ni vizuri suti ikivaliwa na viatu vya kufunika miguu na siyo vya wazi,urefu wa kiatu inategemea na mvaaji zaidi kama suti ni fupi basi kiatu kiwe kirefu
Alisema kuwa siku hizi kuna watu wamebuni vitu vya kuongezea katika suti ili ionekane vizuri na inavutia machoni mwa watu
Suti inaheshima yake na ndio maana wengine wanaendelea kuvaa harusini na wengine katika hafla mbalimbali za kitaifa