WASANII WALALAMIKIA UTARATIBU WA KUPATA KILAJI
Utaratibu wa wasanii kutoka kwa pamoja na kwenda kunywa baada ya kutoka sehemu wanayoifanyia kazi 'location' umezua utata baada ya baadhi ya wasanii kudai utaratibu huo unawatenga wale ambao hawatumii kilaji na kukosa ushirikiano kwa wezao
Chanzo chetu cha habari cha kuaminika kilieleza kuwa hatua hiyo imechangia baadhi ya wasanii kuonesha kusikitishwa na utaratibu huo kwani wanatengwa bila kuzingatia maoni ya mtu
"Nashindwa kuwaelewa kwani wanachokifanya siyo kizuri unapotoka 'location' mtu unatakiwa urudi nyumbani kwa ajili ya kupumzika lakini wao wanataka tukakae bar tuanze kunywa pombe na unapokataa basi wewe si mshirika wao" kilibainisha chanzo hicho
Pamoja na hayo chanzo hicho kilibainisha kuwa maisha wanayoishi baadhi ya wasanii wengi wa hapa nchini hususani wakinadada ni ya kuigiza na si maisha yao ya halali
Chanzo hicho kiliendelea kusema kuwa maisha wanayoyaishi baadhi ya wasanii wengi wa hapa nchini hususani wakina dada ni ya kuigiza na si maisha yao halisi hali inayochangia kufanya masuala ambayo yapo kinyume na maadili
Katika hatua nyingine msanii anayeigiza sauti za viongozi na pia ni msanii wa filamu nchini Steve Nyerere alikana kuwepo na tabia hiyo kwa wasanii wa Bongo Movi
Alisema kuwa si ukweli kwamba wanapotoka katika shughuri zao za sanaa na kuingia bar na hata kama ipo si kweli kama wanalazimishana kuhudhuria vikao kama hivyo kwani kila msanii anamaamuzi yake
Kwa upande wa wasanii wanaoishi maisha ya kuigiza mwenyekiti wa nidhamu wa Klabu ya Michezo ya Waigizaji wa Bongo (Bongo Movie), Heriety Chumira alisema kuwa ni kweli baadhi ya wasanii wanaishi kwa kuigiza
Alisema kuwa kinachowaumiza kutotaka kuishi maisha yao halisi na kuhitaji maisha ya juu ili aonekane kama yuko juu kitu ambacho ni kibaya kwa maisha yao
"Movi hazilipi kiasi kikubwa ambacho unaweza ukamiliki gari na nyumba ya kifahari, hivyo unatafuta njia za ajabu ili waweze kumiliki vitu vikubwa" alisema