MAAJABU YA WACHEZA SHOO WA JB MPIANA
Mcheza shoo wa bendi kongo ya muziki wa Wenge BCBG akishambulia jukwaa kwa mtindo wa kipekee baada ya kuvua nguo zote jukwaani na kubakiwa na chupi tu
Pamoja na kuchelewa kuanza shoo hiyo kutokana na matatizo ya kukatika kwa umeme kila muda JB Mpiana pamoja na kundi zima la Wenge BCBG walishambulia jukwaa hilo na kusababisha mashabiki kusahau tatizom la kukatika kwa umeme mara kwa mara ingawa mwanamuziki huyo alipokuwa jukwaani hakupata na tatizo hilo la umeme kukatika
Katika shoo hiyo JB Mpiana aliweza kupiga nyimbo mbalimbali za zamani ikiwa pamoja na Barakuda, Djodjo Ngoonda, Walay Danico, Dizo Dizo na zile mpya katika mtindo wa non- stop
Katika onyesho hilo Mashujaa ndio walikuwa wa kwanza kupanda jukwaani kwa ajili ya kufanya shoo ya ufunguzi lakini walishindwa kufika mwisho wa shoo hiyo kwa kukatika kwa umeme huku ukichukua dakika 30 katika utengenezaji
Tatizo hilo liliendelea mara kwa mara huku bendi hiyo ikishindwa kumaliza nyimbo hata moja