MAMA YAKE RAY C AKANUSHA UVUMI WA KIFO CHA MWANAYE
Wiki kadhaa baada ya kuwasili nyumbani kwao uvumi ulizagaa kwamba muimbaji aliyepata umaarufu mkubwa katika ukanda wa Afrika Mashariki Rehema Charamila maarufu kwa jina la RAY C au 'kiuno bila mfupa' amefariki uvumi ulizagaa nchini Tanzania katika mitandao ya kijamii
Uvumi huo umehamia Kenya hata hivyo mama yake Ray C alikanusha habari hizo katika mahojiano na kituo cha radio cha Kenya cha Citizen Radio kupitia kipindi 'cha mambo Mseto' kwamba taarifa hizo si za kweli na kwamba mwanaye yupo hai na anaendelea vyema na matibabu yake