RAPA maarufu ambaye ni zao la Bongo Star Search Kala Jeremiah amekuja na mapinduzi ya aina yake kwa kuamini kuwa albamu inalipa zaidi kama ukiwa umejipanga katika kupambana na mauzo hayo
Akizungumza na mwandishi wa habari hii juu ya uzinduzi wa albamu yake mpya inayokwenda kwa jina la 'Pasaka' itakayozinduli usiku wa siku ya Jumapili
Kala alisema kuwa, anapambana yeye mwenyewe katika mauzo ya albamu yake na mpaka sasa teyari ameshauza nakala kadhaa kila akifanya shoo
"Albamu hazilipi kama unampelekea muhindi akuuzie kwani hizo shilingi miambili kuziweka mpaka zitimie milioni kadhaa ni safari ndefu, ila ukiingia mwenyewe mzigoni ni utaona faida yake kwani" alisema Kala
Nyota huyo aliidokeza Maisha kuwa anauza albamu yake taratibu taratibu huku akiwa na faida tofauti na kuwategemea wahindi wakufanyie biashara ingawa kwa sasa tepu sokoni hazina nafasi tena, zenye nafasi kubwa ni CD peke yake
Nyota huyo ambaye ameibuka katika mashindano ya kusaka vipaji ya Bongi Star Search, atazindua albamu yake Januari 13 huku akisindikizwa na wasanii wakali kama Roma, Bden Pol, Jokate a.k.a. Kidoti ambaye ameshirikishwa katika kiitikio cha wimbo wa 'Ningekuwa Rais uliomo kwenye albamu hiyo