STEVE NYERERE NDIYE ALIYESABABISHA USHINDI WA DK. MAHANGA
NAIBU Waziri wa Kazi na Ajira DK.Mahanga ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Tabata Segerea amejikuta akifichua siri nzito ya ushindi wake wa ubunge jimboni hapo
DK. Mahanga ambaye amejikuta akieleza kilichosababisha ushindi wake ni kutokana na kampeni kubwa zilizofanywa na msanii wa filamu nchini Steve Nyerere
Alisema hayo wakati akitoa salamu zake za rambirambi kwenye familia ya Sajuki wakati alipotakiwa kutoa mchango wake wa ili kuwezesha shughuri za mazishi kufanikiwa
Alisema kuwa, katika kipindi chote amekuwa akishirikiana kwa asilimia kubwa hususani katika harakati za kampeni, hivyo anamshukuru Steve Nyere kwa kujitoa kwake na kuweza kufanikisha ushindi wake kwa kishindo
"Steve Nyerere amekuwa ni mtu muhimu sana kwangu kwa kuweza kufanikisha kampeni na wananchi walimuelewa kila alipopanda jukwaani kuhamasisha swala la upigaji kura hivyo naikubali kwa asilimia kubwa sana kazi yake" alisema Mahanga
Pamoja na hayo pia alisema kuwa anasikitika kumpoteza mmoja wa mpiga kura katika jimbo lake, na mwanaharakati wa ajira kwa vijana kwani kupitia kazi yake aliweza kutoa ajira kwa vijana wenzake na yeye mwenyewe kuweza kujiajiri