Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa kwenye mitandao zinaeleza kuwa mpelelezi huyo alisema taarifa za hospitali zilidai kuwa kifo chake kilitokana na kuzama kwenye maji wakati akioga na ugonjwa wa moyo baada ya kutumia dawa za kulevya kwa wingi
Alisema baada ya wataalamu kuufanyia uchunguzi mwili yake walidai kuwa walimkuta mfumo wake wa damu ukiwa na kiwango kikubwa cha dawa za kulevya aina ya cocaine lakini mwili wake haukuwa na jeraha lolote
Mpelelezi huyo alisema kuwa amefanya upelelezi na anao ushahidi unaonyesha kuwa nyota huyo aliuwawa na kifo chake hakikutokana na ajali ya kuzama katika maji baada ya kubwia dawa za kulevya
Mpelelezi huyo alikabidhi vielelezo vya ushahidi huo ambavyo vinaonyesha mwimbaji huyo aliuwawa kutokana na deni la fedha za dawa za kulevya zipatazo dola za Marekani milioni 1.5
Alisema ushahidi huo unaonyesha majeraha wakati nyota huyo akiwa anapambana na mashambulizi hivyo anaamini kuwa nyota huyo alishambuliwa na mtu waliyekuwa anamdai fedha hizo wakati akiwa katika hoteli hiyo
Haikuwa mara ya kwanza wafanyabiashara wa madawa ya kulevya kushambuliwa ili kulipa deni wanalodaiwa
:Kwa mujibu wa mitandao mbalimbali ya kimataifa