MWAKIFAMBA: KIKWETE ANAWAJALI WASANII
Imeelezwa kuwa Rais wa awamu ya nne Jakaya Kikwete amekuwa mstari wa mbele kujitoa kwa wasanii katika matatizo yao hali hiyo inayochangia wasanii wa filamu kuona kuwa rais anawajali na kuthamini mchango wao katika taifa
Hali hiyo imejionyesha pindi wasanii wa filamu wanapopata na matatizo ya kuugua hata msiba, rais anapokuwa karibu nao bega kwa bega
Hayo yalielezwa na Rais wa Shilikisho la Filamu Tanzania (TAFF) Simon Mwakifamba kwa kuonyesha kukubali kazi na ushirikiano wanaoupata kutoka kwa rais Kikwete
Alisema kuwa Rais wa awamu ya nne amekuwa mstari wa mbele kuwasaidia wasanii hali hiyo imetuonyesha kuwa rais anatujali pamoja na kuthamini kazi yetu
"Huyu ni rais wa kwanza kujali wasanii kwa kiasi kikubwa sana, amekuwa mstari wa mbele kuwasaidia, hata kwenye ugonjwa wa Sajuki yeye ndiye aliyekuwa amsafirishe India kwa ajili ya matibabu, hivyo tunajivunia rais huyu kwa kitendo chake cha kuwajali wasanii" alisema Mwakifamba
Mbali na hayo pia amekuwa ni rais wa kwanza kuongoza maelfu ya watu kumzika msanii Sajuki, hali ambayo imeonyesha faraja kubwa kwenye familia ya wasanii wa filamu nchini