MPOTO AWASHUKIA WASANII WANAOIGA KAZI ZA NJE
Kutokana na baadhi ya wasanii kutokuwa na mtazamo juu ya muziki na kukumbwa na hali ya kutofahamu muziki unataka nini kwa hali iliyopo hivi sasa inapelekea kuwa sababu moja wapo ya kushindwa kufanya vyema katika ngazi ya kimataifa
Baadhi ya wasanii wanajikuta wanaimba kulingana na mazingira waliopo na si kujua soko la kimataifa linataka nini hali hiyo inasababisha kuendelea kudumaza muziki wetu
Msanii maarufu wa ushairi Mrisho Mpoto 'Mjomba'amefunguka hayo jijini Dar es Salaam wakati akitoa maelezezo ya kutokuwa na uhusiano wowote kati ya lugha na ukuaji wa muziki
Mpoto alisema kuwa hakuna uhusiano uliopo kati ya ukuaji wa muziki pamoja na matumizi ya lugha ya kiswahili, kwani waimbaji wengi maarufu barani afrika wamepata umaarufu kwa kuimba lugha za kwao
"Wasanii wengi kama kutoka South Afrika wanatumia lugha za kwao na wanafanya vizuri kwenye anga za muziki wa kimataifa hivyo hakuna uhusiano wa lugha katika maendeleo ya muziki ila hapa tanzania wasanii wanatakiwa wajipange na si kukulupuka" alisema Mpoto
Alisema baadhi ya wasanii wa hapa nchini wamekosa maudhui na kusababisha kupoteza ladha na maana ya muziki mbali na hilo pia wamefikia hatu ya kuiga kazi za watu kitu ambacho kinadidimiza sanaa ya muziki
"Wasanii wengi wanakurupuka kama mtu anampenzi wake mwajuma wa mtaa wa pili kesho utasikia anaimba kuhusu mwajuma lakini soko la muziki katika ngazi ya kimataiafa halitambui hilo na hapo ndipo tunapofeli kila siku" alisema Mpoto