MWANAMUZIKI WA BONGO ANAYEFANYA KWELI NCHINI SWEDEN
Mwanamuziki wa kizazi kipya nchini Tanzania Janbert Kiwia 'JanB'anayefanya muziki wake nchini Sweden amekamilisha ujio wake wa albamu yake ya kwanza inayokwenda kwa jina la 360 kwa mwaka
Akizungumza jijini Dar es Salaan JanB alisema kuwa teyari ameshaachia video za nyimbo mbili Pretty Girl na Play haters ambazo zote zinachezwa channel O na katika vyombo vya habari nyingine Afrika Mashariki
Alisema kuwa anafanya muziki wa kileo na anaangalia nini kinatakiwa katika soko la muziki na ndio maana video zake zinafanya vizuri katika ngazi za muziki za kimataifa
Akizungumzia kwa nini video zake zinachezwa channel O tofauti na baadhi ya wasanii walio wengi Tanzania alisema kuwa, kuchezwa kwa video zake channel o ni kutokana na ubora uliopo kwenye video zake
"Video zangu zina ubora wa kimataifa na ndio maana imekuwa ni lahisi kuchezwa channel O ingawa napata shida sana kwa hapa nyumbani bado watu hawajaelewa kazi zangu" alisema JanB
Aliongezea kuwa anajipanga ili aweze kuendelea kufanya vizuri zaidi kwenye gemu la muziki ingawa anaomba ushilikiano kutoka kwa watanzania ili aweze kufanikisha malengo yake