NICKI MINAJ NA MARIAH CAREY HATIMAYE WAMALIZA' BIFU' LAO
Inaelezwa kwamba hiki walichosema ni uongo au bifu lao lilikuwa ni la uongo Nicki Minaj na mwanamuziki mwenzake Mariah Carey wamesema kuwa bifu lao lilikuwa ni la ukweli na sio la kutunga
Walipoulizwa ni namna gani wameweza kusahau bifu lao hilo, Mariah alijibu, "muda huponya majeraha yote."
Majibu hayo ya Mariah yanaacha mashaka kwa watu kwa kuwa si muda mrefu umepita kiasi cha kuweza kuponya bifu hilo kali lililoshuhudiwa miezi michache iliyopita
Minaj, ambaye amelipotiwa kuwa alikuwa amekaa kama vile haelewi kitu aliongeza kwa kusema, "Na tuliangalia mkanda wangu wa sex," akidokezea kuhusu mkanda wa mapenzi ambao umekuwa ukizungumziwa kwa miaka mingi "Sisi ni watu wenye taaluma yao Umewahi kugombana na mtu ambaye unafanya nae kazi." alihoji Minaj
Carey na Minaj walikuwa waliyasema hayo wakati wakihojiwa katika shoo ya kusaka vipaji vya kuimba, ambapo wawili hao ni miongoni mwa majaji wa shoo hiyo.
Carey alisema taarifa za bifu lake na Minaj ni usumbufu kwa shoo hiyo na kwa washiriki huku akisema kuwa shoo ya Idol ni kubwa kuliko kitu chochote cha kijinga.
Mwanamuziki huyo pia alisema kuwa yeye na Minaj walishawahi kutoa nyimbo kwa pamoja iliyoitwa Up Out My Face ambayo ilikuwa katika albamu yake ya mwaka 2009 inayoitwa Memoirs of An Imperfect Angel. "Ilikuwa ni moja kati ya nyimbo ninazozipenda na toka siku hiyo nilihisi kuwa Minaj atafika mbali na bado nahisi hivyo." alisema Minaj
Alipoulizwa kama bifu hilo lilipikwa ili kuifanya shoo hiyo iwe ya kuvutia, Raisi wa Fox Mike Darnell alisema, "Carey na Minaj hutofautiana kuhusu vipaji vingi. Sio tu kuhusu wasichana wanaoshiriki, bali ni kwa kila mtu."