Mzazi wa aliyekuwa mwigizaji na mtayarishaji wa filamu nchini marehemu Juma Kilowoko ‘Sajuki’ mzee Issa Juma amesema kuwa amepokea kifo cha mwanaye kwa masikitiko makubwa kwani kabla aliongea na mwanaye kuwa iwapo hali bado inaendelea hivyo arudi Songea mara moja wafanye Tambiko.“Mwanangu ameumwa sana na niliona wazi suala hilo kwa Hospitali kama limeshindikana niliongea na Juma nikwamwambia kuwa arejea Songea ili tujaribu kumfanyia matambiko, lakini akaniambia kuwa ngoja akirudi Arusha katika tamasha lake, lakini kwa bahati mbaya akazidiwa na kurudishwa Dar na kulazwa hadi umauti unamkuta,”anasema Mzee Issa.Mzee Issa alifafanua ni Tambiko gani ambalo lilitakiwa kufanywa kule Songea ilikuwa ni kusomwa kwa Dua baada ya baba wa msanii huyo kuwaita Masheikh na kusoma Dua, Sajuki alifariki siku ya Jumatano asubuhi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alipokuwa amelazwa kwa maradhi ya saratani ya Ngozi na matatizo ya mgongo.Marehemu ameacha mke na mtoto mmoja wa kike
INNA LILLAH WAINNA ILAIH RAAJIUN.