Mwanamama Athiya Shetty amewapigia magoti mashabiki akiwataka wasimwite mbunifu wa mavazi bali ni mwigizaji.
Mtandao wa The Times of India,uliandika hivi karibuni kuwa mrembo huyo ambaye ni mtoto wa Suniel Shetty ,alifikia uamuzi huo baada ya mashabiki kudai anatafuta umaarufu kupitia mavazi.
Shetty anayetamba na filamu ya Sonam alisema,sina mpango wa kazi hiyo,wala kuutafuta umaarufu wa mavazi na ubunifu ,kwani kipaji cha kuigiza kinanitosha