Pamoja na kuonyesha wazi kuwa team Ukawa, Dayna amesema japokuwa kila mtanzania ana chaguo lake la mgombea au chama, haitakiwi ilete chuki au uadui bali kila mmoja aelewe na kuziheshimu hisia za mwenzake kisha akamilishe kiu yake kwa kupiga kura kwa amani na utulivu na kuendeleza sifa ya amani iliyokuwepo kwa kitambo’
Dayna amesema Kila Mtanzania ana haki ya kufanya kile nafsi yake inachoamini sio kwa kulazimishwa, mimi naamini ninachokifanya nafsi yangu imeridhika naamini niko huru na sehemu ambayo ina amani, siwezi kukuchukia sababu eti wewe upo CCM mimi niko UKAWA….. hapana, hata ninapokuwepo kwenye kampeni simlazimishi mtu kuja UKAWA, ninachofanya ni kuwaelewesha watu tu wakielewa sawa….‘