Baraza la sanaa la Taifa BASATA linatarajia kutoa Tuzo tano kwa wasanii waliochangia jamiii na waliotumia maisha yao yote katika maendeleo ya sanaa Nchini
Tuzo hizo zitatolewa katika maadhimisho ya siku ya wasanii yatakayofanyika Desemba 12 katika ukumbu wa Blue Pearl uliopo jijini Dra es salaam
Mkurugenzi wa ukuzaji masoko Nsao Vivian alisema lengo la maadhimisho hao ni kutambulisha msanii kazi zake pamoja na mchango wake katika jamii
Naye Rais wa sanaa za maonyesho Tanzania Agnes Lupamba alisema sanaa ina nguvu kubwa katika kubadilisha fikra kwa jamii..