MARIAH CAREY AJIANDAA KUFANYA SHOW KUBWA
Ni Concert kubwa ya sikukuu ya Christmas itakayofanyika ndani ya jiji la New York nchini Marekani. Hili ni tamasha litakaloongozwa na Mwimbaji wa kike mwenye heshima kubwa nchini humo Mariah Carey, ambalo linaitwa “All I Want for Christmas Is You”.
Ratiba ya tamasha hilo itaanza December 8, ambapo Mariah Carey amejiandaa vya kutosha kuhakikisha mashabiki wake wanaenjoy uwepo wake kwenye majukwaa mbalimbali yaliyoandaliwa kufanyika kwa tamasha hilo.
Mariah Carey ambaye kwa muda mrefu hajapanda stejini ataimba nyimbo maarufu za Christmas zilizowahi kutamba miaka ya nyuma huku pia atatumia muda huo kutoa filamu yake inayohusu sikukuu ya crismas.” A Christmas Melody” atakayoitoa December 19.