Jana kuliibuka vita ya maneno Instagram, kati ya rappers Wale na Meek Mill hali iliyopelekea mpaka Meek Mill kutamka wazi wazi ati Wale hayupo tena Maybach Music.
Sasa bosi wa MMG Rick Ross, ameonyesha kwamba yeye ndio ‘mwamba’ na ndio mtu pekee mwenye haki ya kusanua hadharani nani anatoka katika ‘crew’ hiyo.
Ni masaa machache mara baada ya Meek Mill kudai Wale hayupo tena kundini Maybach, Rick Ross amepost ‘clip’ ya Video kupitia ukurasa wake wa Instagram Ikimuonesha Wale akikamua jukwaani mjini Atlanta jana usiku.
Katika ‘clip’ hiyo ya Sekunde 15, Rozay aliipa Caption ya ‘Never Question the Empire’.