Google PlusRSS FeedEmail

DAVIDO KULIPWA DOLA 14?

HII si ni tamaa tu au ndio kutafuta? Staa wa muziki kutoka Nigeria, Davido ni miongoni mwa wasanii wa Afrika wenye mafanikio makubwa sana kimaisha na kimuziki akiwa mmoja wa wale wanaopiga pesa za uhakika.

Kutokana na mafaniko yake, kumekuwepo na tetesi zinazodai kuwa thamani yake kwa sasa inafikia dola14 milioni za Kimarekani  Hata hivyo msanii huyo amekanusha taarifa hizo kupitia kipindi kimoja cha runinga ya MTV Base.

Kupitia Reality shoo hiyo ya R’Real Talk’, Davido aliulizwa na mtangazaji Stephanie Coker kuhusu thamani yake halisi ambapo alijibu kwa kusema, amewasikia ripoti hizo za thmani yake kufikia dola 14 milioni japo si kweli ila anatamani sana kuifikia.

“Niliona kitu kama hicho ila ni uwongo. Dola14 milioni zipo wapi, Dah ila natamani” Davido alijibu.  Tangu aanze kufanya muziki yapata miaka mitatu iliyopita, msanii huyo amekuwa akifanya vizuri sana katika mauzo ya kazi zake nje na ndani ya Nigeria pamoja na kupata shoo kibao kote kote hadi Marekani.

Aidha amejikita katika kufanya kolabo na masupastaa wa Marekani kitu kingine ambacho kimemuongezea umaarufu na kumweka vizuri kisoko

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging