Google PlusRSS FeedEmail

IZZO B 'SIWAUNGI MKONO WANAOWATUKANA WANASIASA'

Rapper kiwango Bongo anayeubeba poa mkoa wa Mbeya Izzo Business, amesema kamwe hatounga mkono vitendo vya wasanii kutumiwa kuwatukana wanasiasa.

Akifunguka kupitia Times FM, Izzo ameeleza kuwa haoni kama kuna ubaya kwa wasanii kwenda kutumbuiza kwenye kampeni kwa sababu ndio kazi zao, lakini tatizo linakuja pale anapotumika kisiasa.

“Sisapoti pale msanii anapoacha kazi zake, na kuanza kuwatukana wanasiasa mitandaoni, inakuwa ameacha kile anachotakiwa kufanya na kuingilia mambo mengine”

Izzo amefafanua na kusisitiza kuwa, kura yake itakwenda kwa Rais mwenye sera mathubuti za kutatua matatizo ya wananchi.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging