Hii imenitokea siku ya Jamomosi tarehe 26 Sept kuamkia Jpili usiku Zanzibar nliweza toka katika Club ambayo twapiga Disco kila siku za Ijumaa Na Jumamosi this time ilikuwa ni katika sikukuu Ya Eid ya Tatu coz Zanzibar huwa kuna sikukuu 4 za Eid,nliweza toka kwa miguu toka sehemu tupigayo Disco Club Bomba mpaka Gymkana Club mida ya saa 7 usiku ambako kulikuwa na show ya Mfalme Berry Black na Yamoto Band as a Radio
Tulikuwa twahusika kama wadhamini wa hiyo show nadhani wengi wenu mliona nlipost picha wakati nawafanyia intervw Wasanii hao na wengine,nliweza fika Gymkana fresh kabisa na wakatika Berry Black anapanda jukwaani na kuona kila kitu kipo sawa nikaamua kuaga na kuanza safari ya kurudi katika Club yetu so wakati natoka tu getini Gymkana nikakutana na mzee ambae alikuwa na pikipiki ndogo nikamwomba lift maana si mbali na hapo akanipa lift na kunishusha barabarani na Club yetu Maisara,Baada ya kushuka tu yule mzee akawa anaondoka ndio ikaja gari aina ya Noah kuna jamaa katika hilo gari akaniita G…
Sikusita kwenda kwani nikajua kuna washkaji wananijua nikawasalimie ila mlango ulivyofunguliwa nikagundua sina ninae mjua nikasalimia na kutaka geuza kumbe kuna mshkaji alikuwa mlango wa mbele wa gari akashuka na kuanza kunipush ndani nipande kwa nguvu Sikuwa nakubali na ghafla gari ikawa inaondoka hivyo hivyo nadhani baada ya kuona hapo sehemu kuna movement nyingi wangeshtukiwa,basi gari ikaenda hadi mbele karibu na msikiti maeneo hayo hayo na kuniachia nikadondoka chini barabarani na gari ikaondoka ikakata kona maeneo ya mbele ya nyumba ya Rais Mstaafu Wa Awamu Ya Pili na mbele yake baada ya makaburi kuna kituo cha Polisi na siku hiyo kulikuwa kimyaa maeneo hayo na taa za barabarani hazikuwa zikifanya kazi ilikuwa
giza,nlivyosimama na kutaka ondoka kujua nipo ok ila mikononi nimechunika ghafla wakaja vijana wenye nguvu hasa na wenye shughuli zao na kunikamata na kuanza nishushia kipigo kama mimi ndio mwizi walinipiga sanasana usoni kama sura muionavyo nlikuwa najitahidi kupiga kelele na wakiona hivyo wananipiga ngumi za mdomoni nikawauliza shida ni nini wakasema wanataka pesa nilizo nazo nikasema kiukweli sikuwa na hela hivyo wakasema mbona mifuko imejaa nikawaambia kuwa ni simu hizo hawakuamini waliendelea kunipiga mwengine alinitight miguu mwengine mikono wengine ngumi tu,mwisho wake nikaja jikuta nimepoteza fahamu kwa muda na baada ya kustuka nikawa naona kama ni ndoto lakini haikuwa ndoto kumbe ni kweli baada ya kujisachi mifukoni kujikuta sina Simu zangu tatu,kipochi,funguo za ofisini na muhuri ambao huwa twatumia katika kazi zetu za nje huku wakiwa wameniachia viatu na saa yangu ya mkononi nikiwa navyo,Mungu mkubwa sana nliweza kutembea japo kwa tabu huku sioni vizuri mpaka sehemu ya Club ili nipate msaaada wa kupelekwa spitali nikafika na baada ya kufika nliishiwa nguvu kabisa tena na nikabebwa na kwenda Polisi kwanza kupata pf3 na baadae spitalini na kupata matibabu ya mwanzo na kulazwa nikiwa na hali mbaya kichwani hizi picha ni siku nlotoka spitali hapo ndio kidogo afadhali,nawakati nipo spitali kuna watu wengine waliletwa wamekatwa mapanga na mwengine kakatwa kidole,nina hofu kubwa sana na Zanzibar kwa sasa kwa hali hii,TUWE MAKINI JAMANI NDUGU ZANGUNI Na Unguja Yetu Hii…
Asanteni Sana Woote Mliokuja Niona Spitali Na Nyumbani Na Pia Mliopiga Simu Japo Sikuwa Naruhusiwa Kuongea Na Simu Lakini Pole Zenu Nimezipata…
Ma Family Yote Ndugu Jamaa Na Marafiki Wooote Maana Kwa Majina Ni Wengi Sana Sana Sio Chini Ya Watu 200,Wengi Mmenichangia Kwa Fedha,Wengine Matunda,Chakula Na Simu...
Namashukuru Allah Kwa Kila Kitu Kwa Kuniweka Hai Na Kuninusuru Na Janga Hili Naendelea Vizuri...Alhamdullilah...