MANENO YA ICE CUBE BAADA YA NWA KUTAJWA KUWANIA ROCK
Rapper Ice Cube ametoa tamko baada ya ‘Crew’ yao ya kitambo ya Hip Hop N.W.A, kutajwa kuwania tuzo za Rock & Roll hall of fame kwa mara ya pili.
Cube anasema anajisikia vizuri na faraja kuona mchango wa N.W.A, unatambuliwa na kuheshimika kwenye ulimwengu wa muziki.
“Ni kitu kikubwa kiukweli kwa mwaka huu, hii inatupa nguvu kila siku kuendelea kufanya vizuri, na hii ni moja kati ya kudumisha ndoto za Easy E” alisema Ice Cube.
Wengine waliotajwa kuwania kipengele kimoja na N.W.A ni Janet Jackson, Nine Inch Nails, the Smiths, Deep Purple, Chic, Steve Miller, Chicago, Chaka Khan, the Spinners, Cheap Trick, the Cars, the J.B.’s, Los Lobos na Yes.