Ndoa ya mwanamitindo na mtangazaji wa vipindi vya televisheni huko Marekani,Khloe Kardashian na mume wake Lamar Odom haikuvunjwa rasmi
Lamar anapigania uhai wake Hospital baada ya kuzidisha matumizi ya dawa za kulevya alizozitumia kwa muda wa siku nne mfululizo
Mke wa nyota huyo huyo wa zamani wa ligi kuu ya kikapu ya Marekani NBA Khloe amenungana na mumewe kuhakikisha anapona
Mrembo huyo amesema ameamua kuungana na mumewe katika kipindi hiki kwa kuwa ndoa yao haikuvunjwa rasmi ila walikuwa wametengana na mumewe baada ya kuonekana kuwa anatoka nje ya ndoa na matumizi ya dawa za kulevya
Nyota huyo alisema walikubaliana kuvunja ndoa yao mwaka jana na julai mwaka huu walitia saini mkataba wa kuvunja ndoa lakini haikuwezekana kwa kuwa mahakama haikudhibitisha
Khloe na Lamar bado ni mke na mume kisheria kwa mujibu wa sheria kwa kuwa ndoa hiyo haijavunjwa kisheria kama walivyokubaliana