First Lady wa Kundi la Tip Top Connection lenye maskani yake pande za Manzese, Dar es Salaam, Khadija Shaban a.k.a K-Sher amesimamishwa kupiga mzigo ndani ya kundi hilo kwa kipindi kisichojulikana.
Nondo zinaangushwa moja kwa moja na meneja wa kundi hilo, Khamis Tale Tale a.k.a Babu Tale kwamba wamefikia uamuzi huo baada ya K-Sher kuonesha utovu wa nidhamu kitu ambacho kimekuwa kikiwapa usumbufu kwa muda mrefu.“
Mara nyingi K-Sher amekuwa akifanya vitu ambavyo vinaleta usumbufu kwa wenzie, mfano hivi karibuni tulikuwa na shoo Mwanza, yeye alishindwa kufika kwa sababu tulishindwa kupata tiketi ya ndege kwa muda huo, wenzie walikuja kwa basi na kufanya shoo kisha kurudi Dar.
Tulipofika Dar akawa anadai alipwe pesa za shoo hiyo, huku akitishia kujitoa kundini kama hatukufanya hivyo, siyo hilo tu yapo mengi ambayo msanii huyo amekuwa akiyafanya na kusababisha usumbufu kwa wenzie kitu ambacho kimetusukuma sisi viongozi kuchukua uamuzi wa kumsimamisha mpaka hapo baadaye,” alisema Tale.