Hv karibuni kulikuwa na minongono ya kana kwamba mwanadada na pia mwanamuziki Beyonce alikuwa na kutoelewana kati yake na baba yake,
kutoelewana huko kwa mwanamuziki huyo na baba yake Mathew Knowles kulimpelekea mwanadada huyo kumkabizi mikoba ya umeneja mumewe Rappar Jay Z,
Wakati hayo yanaendelea kampuni ya kusimamia kazi za wanamuziki Music World Entertainment imeweka wazi kuwa wawili hao bado wako katika mahusiano mazuri ya kibiashara na Mathew Knowles ndiye meneja pekeee wa Beyonce na si kama baadhi ya vyombo vya habari vilivyoripoti uvumi huu..