Google PlusRSS FeedEmail

SASA MOTO UNAKARIBIA KUWAKA KEISHA AJIBU MAPIGO YA BAB TALE


Zengwe ndani ya kundi la muziki wa kizazi kipya la Tip Top Connection lenye maskani yake Manzese Jijini Dar,Bado linaendelea kama mchezo wa kuigiza,story kubwa juu ya First Lady wa kundi hilo,Khadija Shaban a.k.a K-Sher amejitoa au amefukuzwa na hapa Keisha ameibuka na kumwaga mapya manne..

Akichonga na pro 24 kwa njia ya simu mwanadada K-sher alisema kiongozi wa kundi hilo Babu tale anatakiwa aongee ukweli kwani anacho anachoficha mbele wa wadau wa mziki wa kizazi kipya,kuna mambo manne ambayo wapenzi wa muziki nataka kuwaeleza..

Kwanza siwezi kufukuzwa Tip Tip kwa sababu uwezo wangu unajulikana ,ukweli ni kwamba nikitoka ,basi kundi litayumba sana ,kwa sababu nina mchango mkubwa kimuziki katika Tip Top,
Sijafukuzwa mimi nimejitoa mwenyewe na sababu kubwa ni kwamba sina imani na uongozi

Babu Tale asiongee uongo na kama wanahitaji nirudi,sharti la kwanza ya mazungumzo mengine,Babu tale anatakiwa anilipe pesa zangu 480,000/= ambazo ni madeni ya pesa alizokuwa akinisainia baada ya shoo na kuniletea pungufu,

Vile vile siwezi kulumbana na hao kwa sababu nina mambo mengi ya kufanya kwa ajili ya kukuza uchumi wangu binafsi, na taifa langu kwa ujumla alimalizia kwa kunena hayoooooo.. 






This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging