Google PlusRSS FeedEmail

BAADA YA LIL KIM KUDAI ATAITANGAZA BONGO HUKO KWAO NAYE MS TRINITI AFATA NYAYO..

Baada ya mwanadada kutoka marekani Lil Kim kudata na Bongo na kuweka wazi ya kuwa katika albamu yake atahakikisha anamshirikisha mwanamuziki nguli kutoka Tanzania Juma Kassim Kiroboto,katika baadhi ya nyimbo katika albamu yake ijayo..
Wakati Watanzania wakiwa wanasubiri shavu kutoka kwa msanii huyo wa Kimarekani tayari mwanamuziki kutoka Trinidad and Tobago Ms Triniti  Kupitia kwa wakali wawili wa muziki wa Bongo Fleva, Ambwene Yesaya ‘A.Y’ na Ilunga Kharifa ‘Cpwaa’ upo uwezekano mkubwa kwa mwanadada Ms. Triniti mwenye asili ya Trinidadi na Amerika kuipeperusha  Bendera ya Bongo mbali zaidi.

Kauli hiyo ilithibishwa na A.Y alipokuwa akigonga ishu mbili tatu na kusema kolabo aliyofanya na staa huyo wa kimataifa huenda ikazaa matunda kwa wasanii wa Bongo kupata dili nyingi katika nchi za mbali.

“Nimefanya naye ngoma yenye jina la ‘Goog Look’ ambayo video yake tumepiga Uganda, naamini ataipeleka mbali zaidi na kutufanya Wabongo tutambulike kimataifa,” alisema Ambwene.

Msanii mwingine aliyepiga kolabo na Ms. Triniti aliyekuja Bongo hivi karibuni kwa ajili ya shoo kadhaa ni ‘Cpwaa’.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging