Google PlusRSS FeedEmail

JE NI KWELI MAN DOJO ASEKWA LUPANGO?

Wakati Domo Kaya ameachia ngoma yake inakwenda kwa jina la mamiss ngoma ambayoinazungumzia walimbwende ambao huwa wanaiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Dunia,

Ipo stori inayovuma kwamba Mandojo ambaye kwa pamoja na domo kaya waliwahi kufanya vizuri katika mziki huu wa kizazi kipya hasa kupitia wimbo wao ‘Nikupe"  Joseph Michael ‘Mandojo’ yupo jela huko kanda ya kati  Singida

Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vinasema  kwamba msanii huyo amefungwa miaka miwili jela lakini haijabainika ni kisa gani ambacho kimemfanya kupelekwa jela.
Mshirika wa Mandojo, Precioust Juma ‘Domokaya’ wiki iliyopita  alibainisha ya kuwa hata yeye amesikia uvumi huo ila bado hajaipata fresh, anachojua ni kwamba mchizi yuko nyumbani kwao Manyoni, Singida kwa ajili ya matatizo ya kifamilia likiwemo lile la kufiwa na baba yake mzazi. “Mi pia sijui chochote kuhusu hilo kwa sababu sijapata simu au taarifa yoyote kutoka huko, siwezi kulizungumzia hilo sana,” alisema Domo.

Tangu wiki iliyopita habari zimekuwa zikizagaa jijini kuwa mchizi huyo ametupwa lupango kwa miaka 2.

Hata hivyo wasanii mbalimbali wakubwa pia wanazungumzia  kwamba Mandojo ameingia kifungoni kwa kosa la kupigana hadharani na watu wasiojulikana

Pro-24 inaendelea kufuatilia kwa makini habari za bingwa huyu na itakuwa ikiku-update kila inapopokea habari mpya..

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging