Jaji mkuu wa BSS, ‘Madame’ Rita Paulsen, amemtania Jaji mwenzake, Salama Jabir, kuwa tangu atoke Ulaya sasa amekuwa na upeo mkubwa.
“Salama, Ulaya wamekusaidia sana , siku hizi umekuwa na ‘sense’,” alisema Rita mara baada ya Salama kutoa maoni yake kuhusu mshiriki, Irene Haule.
Irene aliingia stejini na kuimba moja ya nyimbo za Judith Wambura ‘Lady Jaydee’, na baada ya kumaliza, Salama alimpa maoni kwamba, hakuutendea haki wimbo alioimba na kwamba, amemwaibisha Jaydee ambaye Salama alimwita shoga yake na kwamba anafaa kwenda nyumbani.
Salama ameanza kuonekana katika kipindi cha BSS cha wiki iliyopita, kama mmoja wa majaji baada ya kuwa safarini nchini Uingereza kwa muda mrefu kimasomo.
Tofauti na miaka ya nyuma, safari hii amebadilika kwa kiasi kikubwa kwani maneno yake kwa washiriki yamekuwa na staha.
Wakati huo huo, Madame Rita, amewataka washiriki wa shindano hilo kutokatishwa tamaa na maneno ya majaji.
“Wengine ni mara yao ya kwanza hapa lakini wanaongea, kuna watu waliwahi kuambiwa hapa nyimbo zao ni za maiti, sijui nini, lakini walinyakua sh mil. 25,” alisema Rita baada ya Salama kumshushua Saumu Ramadhani.
PRO24 RADIO/TV
CLICK AND ENJOY GOOD MUSIC
MIXTAPES
ARTIST PROFILES
Blog Archive
LOVE LINKS
PRO-24 DJS OFFICIAL BLOG
PRO24 ENTERPRISES. Powered by Blogger.








