Google PlusRSS FeedEmail

MPOTO ASHEHEREKEA SIKU YAKE YA KUZALIWA NA YATIMA

Msanii wa  miondoko ya mashairi nchini, Mrisho Mpoto a.k.a Mjomba, ametoa misaada kwenye kituo cha watoto yatima na wasio na makao maalumu, CHAKUWAMA Orphanage Centre, kilichoko Sinza-Mori, jijini Dar es Salaam ambacho kinamilikiwa na Mama Hadija.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mpoto alisema ameamua kuwasaidia watu hao akiamini kuwa ni jamii yake kwani yeye pia ni yatima na siku ya leo ni siku ya kuzaliwa kwake inayoambatana na tarehe ya kifo cha mama yake mzazi.

“Nimeamua kutoa misaada kwani ni sehemu ya kutambua uwepo wa kundi hili muhimu, hata mimi ni mwenzao kwani sina wazazi na kwa kuwa leo ni siku ya kuzaliwa kwangu na ni siku ambayo mama yangu mzazi alifariki. Hivyo katika hili sina cha kuongeza zaidi ya kuwatia moyo na Mungu atawalinda,” alisema Mpoto.

Mpoto ni msanii aliyepata mafanikio makubwa kutokana na mashairi yake na sasa ameweza kutengeneza bendi yake binafsi inayofahamika kwa jina la ‘Mjomba Band’ yenye makazi yake Kinondoni-Mkwajuni jijini Dar.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging