Google PlusRSS FeedEmail

WATANZANIA WAMNYIMA KURA MWISHO AZIKOSA DOLA LAKI MBILI.

JOHANNESBURG, Afrika Kusini
MSHIRIKI wa shindano la Big Brother Africa All Stars kutoka Tanzania Mwisho Mwampamba jana alikosa kitita cha dola 200,000 baada ya kushuhudia fedha hizo zikienda kwa mshiriki kutoka Nigeria Uti.

Katika shindano hilo ambalo Mwisho ameweza kudumu kukaa katika jumba kwa muda wa siku 91 alikuwa ni mshiriki wa pili kutolewa kati ya watano waliobakia akitanguliwa na mshiriki kutoka nchi ya Kenya Sheila.

Washiriki wengine waliotolewa na kumuacha Mnigeria huyo akijizolea kitita hicho ni pamoja na Lerato ambaye alikamata nafasi ya tatu huku mshiriki kutoka kwa Mugabe yaani Zimbabwe akiwa mshiriki wa mwisho kutolewa na kumuacha Uti peke yake ndani ya jumba kama mshindi wa mihela hiyo.

Ili mshiriki apate ilikuwa ni lazima apate kura nyingi kutoka katika nchi tofauti ambapo Tanzania ilionekana uzalendo umetushinda kwani hatukumpigia kura mshiriki wetu hivyo hakupata kura hata moja kutoka katika nchi yoyote hali ilikuwa kama hivyo kwa mshiriki kutoka Kenya Sheila na Afrika Kusini Lerato.

Kura zote zilienda kwa washiriki wawili ambao ni Uti na Munya ambao walipishana kwa kura moja ambapo Uti alipata za nchi 8 ambazo ni
 
Wakati Munya alipata kura 7 ambapo nchi zilizompa kura ni Botswana, Malawi, Namibia, South Africa, Tanzania, Zambia and Zimbabwe.Angola, Ethiopia, Ghana, Kenya, Mozambique, Nigeria, Uganda and the Rest of Africa.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging