Google PlusRSS FeedEmail

KANDI WA XSCAPE AFUFUKA AJA NA MAKALI MENGINE KUANZIA DESEMBA 14

Mwanamama aliyetesa sana katika miaka ya Tisini hasa alipoachia kibao chake Dont think im not..Mwanamama Kandi Burruss ambaye alishawahi kuwa ni mmoja kati wadada waliokuwa wakiunda kundi la XSCAPE,

Ameweka bayana kurudi kwake katika ulingo wa muziki kwa mara nyingine,mara baada ya kuwa kimya kwa muda mrefu sasa..Kandi ameweka bayana hayo katika ukurasa wake wa twitter akisema kuwa Desemba 14 mwaka huu ataachia Albamu yake mpya ambayo ameibatiza jina la Kandi Koated..

Katika kujiweka sawa mwanamama huyo atawashirikisha wanamuziki wenzie kutoka katika kundi lake la zamani na wanatarajia kufanya show nyingi katika miji kumi na miwili ya Huko Marekani..iliongeza wasanii wengine ambao atakuwa nao katika mzunguko huo ni rafiki yake kipenzi Fantasia.na  Bwana mkubwa Eric Benet


Aliongeza tayari ana ngoma moja aliyofanya na Fantasia na ngoma ambayo itaachiwa wiki hii na jina la ngoma hiyo ni Back to me..

Kandi alishawahi kushinda Tunzo za Grammy na hakika ujio wake huu utakuwa na mafanikio makubwa...

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging