Google PlusRSS FeedEmail

"SITAKI KUUMIZWA" YA SAJNA NI MUENDELEZO WA STORY YA IVETA

Sitaki Kuumizwa ya Sajna akiwa amemshirikisha Bibie Linah wa Tht ni muendelezo wa ngoma yake ambayo inafanya vyema kunako game ya Bongo Flever ,katika ngoma hiyo verse zote hadi za Linah zimetungwa na Sajna, ila chorus ndio katunga Linah mwenyewe. Ila upande wa ngoama yake Iveta wimbo mzima ailiutunga Sajna mwenyewe.

Hii sitaki kuumizwa ni mwendelezo wa stori ya iveta , ukiusikiliza kwa makini utauelewa, ila kwa ufupi ni kwamba yule binti Iveta baada ya kuachwa muda mrefu kule kijijini na mpenzi wake alieenda mjini kutafuta maisha,
Wazazi wa Iveta walimlazimisha aolewe na jamaa mwingine mwenye pesa alieenda mpaka huko kijijini kumchumbia, japo Iveta alikuwa bado anampenda yule jamaa yake wa mwanzo ambaye alikwenda mjini kutafuta maisha ila ikabidi afate maamuzi ya wazazi akaolewa na huyo bwana mpya mwenye pesa na akampeleka mjini kuanza maisha mapya

Baada ya miezi kadhaa yule mpenzi wa mwanzo wa Iveta akawa na maisha kule mjini akaona sasa ni wakati muafaka kumfata Iveta kijijini ili warudi wote na kuishi mjini. Alipofika kwao kijijini,akakuta iveta ameshaolewa na yuko mjini akaanza kutokwa machozi baada ya kuambiwa Iveta ameshaolewa na mwanaume mwingine, ikabidi tu arudi zake mjini...

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging