Msanii Sam wa Ukweli, maarufu kwa kibao chake cha mgeni wa mapenzi, amekanusha vikali minong'ono inayoendelea chini chini mitaani kuwa yeye ni msanii mwenye maringo kiasi kwamba hataki kushirikiana na wasanii wenzake hata wakati wa kula msosi.
Akikanusha habari hizo Sam alisema jambo ama tukio la yeye kula na wenzanke lilitokana na suala la mkataba wa shoo alizokuwa amesaini kuzifanya kwa siku hiyo ambapo muda ulikuwa haumruhusu kukaa pamoja na wenzake kwa sababu aliwasili Zanzibar mida ya saa tisa na kwenda moja kwa moja kwenye ukumbi wa shoo na baada ya kumaliza kuimba aliwaishwa uwanja wa ndege kurudi bara ili kujiandaa na shoo ambayo nayo alikuwa anatakiwa aifanye usiku huo.
"Mimi nilipata shoo mbili siku hiyo moja ilikuwa alasiri na nyingine usiku. Nilipofika Zanzibar nilipokelewa bandarini na kupelekwa moja kwa moja kwenye shoo kwani nilikuwa nimechelewa hivyo hakukuwa na muda wa kula wala kukaa na wenzangu na hivyo nilivyomaliza nilichukuliwa haraka haraka na kupelekwa katika uwanja wa ndege kurudi Dar-Es-Salaam kwa ajili ya shoo nyingine," Alisema SamAlimalizia kwa kusena, "Nafikiri kama kuna mtu anaona nimemkosea basi nitawaomba anisamehe kwa kitendo kile lakini mimi sina mapozi ya aina yeyote."