Google PlusRSS FeedEmail

TAMASHA KUU AFRICA LIKO TAYARI- ZI FF 2011 YAJA KWA VISHINDO: SHAGGY KUTINGA NGOME KONGWE

Leo ratiba ya tamasha la 14 la ZIFF imetoka ikionyesha kuweko filamu 71 kutoka nchi 39 zitakazoonyeshwa katika siku 10 za tamasha. Pamoja na maonyesho ya filamu kutakuwepo vilevile warsha kubwa 8 zitakazofundisha utengenezaji wa filamu za dokumentari na pia ufundi wa kutumia kamera za HD.
Zaidi ya hayo kutakuwa pia na dhifa kadhaa pamoja na maonyesho ya filamu vijijini yanayodhaminiwa na The Cinema Mondial Tour ya Uholanzi. Filamu hizo pamoja na za ZIFF zitaonyeshwa katika vijiji visivyopungua 15 hapa Unguja na Pemba.

Lakini cha kuvutia zaidi ni kuweko kwa mpiga muziki maarufu Shaggy katika ZIFF. Mjamaika-Mmarekani huyu anajulikana zaidi kwa wimbo wake “It wasn’t Me” uliowakoroga vijana akionyesha utundu wake kimuziki.
“Kwa kweli mwaka huu najisikia sana mimi” alisema Dr Martin Mhando, mkurugenzi wa tamasha la ZIFF. “ Ukiacha Shaggy mwaka huu filamu itakayofungua dimba ni filamu inayohusu muziki na wanawake itokayo Canada/Uganda inayoitwa “Making The Band”. Filamu hii na kuja kwa Shaggy kutatimiza sherehe za Mwaka wa Umoja Wa Mataifa unaosherehekea mahusiano kati ya waafrika walio barani na wale walio nje ya Afrika. ZIFF inahimiza sana mahusiano hayo”
Kwa upande wa filamu, mkazo utakuwa juu ya filamu za dokumentari ambapo mtengenezaji mahiri Nick Broomfield wa Uingereza atakuwa mgeni mashuhuri wa ZIFF. Mtengenezaji huyu wa filamu inayojulikana sana ya “Biggie and Tupac” atakuja kufundisha akisaidiwa na watengeneza filamu wengine kama vile Donald Ravaud (Constant Gardner).
Filamu mpya itakayoonyeshwa mwaka huu ZIFF ni ile inayohusu maisha ya makamu wa rais Maalim Seif Sharif Hamad. Muasisi huyu wa amani na demokrasia hapa nchini anazungumzia maisha yake tangu utoto hadi leo.
Wageni wengine watakaokuja ni Oliver Mutukudzi toka Zimbabwe, anayejulikana kwa muziki wake wakuchezeka na kuliwaza. Filamu 6 zitaonyeshwa kwa mara ya kwanza duniani pamoja na filamu Taka Takata toka Afrika Kusini na The Rugged Priest toka Kenya. Filamu za Waaborijino wa Kiaustralia pia zitapewa umuhimu wa juu katika tamasha mwaka huu.
Itatarajiwa kuwa watu wasiopungua 45,000 watapita Ngome Kongwe katika siku hizo
10 za tamasha.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging