
Kwa mujibu wa gazeti la Daily Mail limetoa taharifa kuwa Mwanamama Cheryl Cole ambaye Mwanamuziki amejipanga vyema kutia maguu katika fani ya uigizaji,huko hollywood.
Cheryl ambaye alikuwa jaji katika shindano la x-Factor amejipanga vyema kuingia katika tansia ya filamu huko hollywood,inasemekana mpaka kufikia katika hatua hiyo kwa sasa ni baada ya kutimuliwa kwake kama jaji katika shindano la X - Factor na Simon Cowell ,
Cheryl anatarajiwa kushiriki kwa mara ya kwanza katika filamu akiwa na waigizaji wakongwe kama Cameron Diaz na Jennifer Lopez katika filamu iliyopewa jina la To Expect when you're Expecting...mpaka sasa mwanamama huyo ameshaanza kupiga picha za video kwa ajili ya filamu hiyo







