
Filamu zilizokaguliwa na kukutwa na ukiukwaji wa maadili ni pamoja na filamu ya Mtoto wa Mamafilamu ambayo ilielekeza kuhamasisha tabia za ushoga kwa kuigiza tabia za kishoga, jambo ambalo linapingana na maadili ya Mtanzania kwa mujibu wa sheria za Tanzania.
Filamu nyingini ni Iny’e, Iny’e Plus, Iny’e Gwedegwede filamu hizi ambazo zimeigizwa na wachekeshaji zimeonekana kudhalilisha wakina mama kwa kuonyeshwa sehemu za miili yao na katika ukaguzi filamu hizi zilipewa daraja la R (Rated R) ambalo filamu zake haziruhusiwi kuonyeshwa katika jamii yetu.







