
Siku za hivi karibuni ilitokea kwa msanii mwenye jina kubwa katika tasnia ya filamu hapa Bongo Mzee Charles Magali ‘Mzee Magali’ alipopigiwa simu na mteja ambaye alikuwa akihitaji kufanyiwa kazi yake ya kuchezewa filamu yake, awali mtayarishaji huyo alisema kuwa alimtuma mwenyeji wa Dar es Salaam aongee na Mzee Magali alisema kuwa alihitaji kiasi cha lakini moja ili aigize katika filamu hiyo.
Lakini alivyopigawa simu baadaye wakati wa kuanza kazi akasema kuwa hawezi kucheza kwa bei ya awali kwani hakujua kama ni nani anayetaka kuchezewa filamu kama ni mtu ambaye si mtayarishaji bei ni tofauti kabisa na lazima aongee na mtu wake. Baada ya kupata habari hiyo tulimpigia Mzee Magali.
“Kwa sasa hauwezi kuongea na mimi kwani nina meneja wangu ambaye ndiyo unatakiwa kuongea naye bwana, yeye ndiyo anaweza kukuelewa kuhusu kazi yako, ongea naye huyu,” analisema Mzee Magali.
Baada ya kuongea na mwanadada huyo alisema kuwa ili kumpata Mzee Magali katika filamu yako ni lazima umlipe laki mbili kwa scene kwa mantiki hiyo kwa scene sita utakiwa kumlipa milioni moja na huduma nyingine kwako, kama ni kweli wasanii kwa sasa wanalipwa hivyo







