Mwanamama Lady Gaga juzi alitumbuiza kukumbuka kijana mwenye umri wa miaka 14,aliyejiua kutokana na kushambuliwa kwa sababu ya vitendo vyake vya ushoga..
Gaga aliimba wimbo wa Hair kumkumbuka kijana huyo huyo Jamey Rodemeyer,ambaye alizikwa huko New York "Kwa mujibu wa Tmz Gaga alisikika akisema , Niliamua kutumia fursa hii kwa sababu tumepoteza kijana tegemeo katika mwezi huu..alisema Lady Gaga juzi usiku mjini Las Vegas."
Kijana huyo aliamua kukatisha maisha yake baada ya wanafunzi wenzake kumdhihaki kuwa ni shoga,inasadikika mazishi ya kijana huyo yalihudhuriwa na watu zaidi ya 500








