Mosun Filani ambaye ni mwigizaji toka huko Nollywood Lagos Nigeria ametangaza rasmi kwamba anatarajia na yeye Kufunga ndoa mnamo mwezo December mwaka huu
Kwa mujibu wa MYJOYONLINE imesema kuwa mtu mmoja wa karibu na familia ya muigizaji huyo aliongeza kwa kusema kuwa mwanamama huyo kwa sasa yuko katika dimbwi la furaha kubwa mara baada ya kupata mchumba ambaye amemuomba kufunga nae ndoa hiyo
Kwa mujibu wa chanzo hicho mwanaume huyo ni mfanyabiashara katika Jiji la Lagos na anajulikana kama Romeo,ambaye ni mwenyeji wa jimbo la Ogun..







