
Mwigizaji maharufu wa huko Hollywood Jessica Chastain,ameweka bayana furaha yake kutokana na kupata nafasi ya kuigiza nafasi ya mtu aliyempenda maishani mwake marehemu Princess Diana.Jessica ndiye aliyeshinda nafasi ya kumwigiza Princess Diana katika filamu iliyopewa jina la Caught in Flight,ambayo imetayarishwa na muandaaji maharufu na mwenye uwezo mkubwa Oliver Hirschbiegel.Filamu hiyo itakuwa ikielezea maisha ya Princess Diana mpaka kifo chake ambacho kilitokea huko Ufaransa kilichosababishwa na ajali ya Gari.Imeelezwa kuwa filamu hiyo itaingia sokoni mapema mwezi March 2012 na zoezi la upigaji picha limefanyika huko Hollywood,Pakistan,Angola,Africa ya Kusini,na Paris Nchini Ufaransa.Jessica Chastain 30 ameshawai kutamba katika filamu kama Texas Killing Fields,Tree of Life na Help in the Dept







