
Mwanamama Wastara Juma anasema hajapotea katika tasnia ya filamu kwani kuna kazi zake zipo sokoni, lakini amewaahidi wapenzi wa filamu zake kuwa amewaandalia filamu kali na ya kusisimua ambayo anasema kuwa itavunja rekodi kwa mwaka huu.Baada ya kutoka na filamu yake na mumewe Sajuki ya Mchanga na Keni, filamu ambayo imefanya vizuri sokoni, pia anatarajia filamu yake ya Kijacho itafunika filamu nyingine zinazoingia sokoni.







