Google PlusRSS FeedEmail

TUMEADHIMISHA MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA BARA BILA WASANII WA FILAMU KUTOJITAMBUA

Kila ninapoangalia runinga au kusoma magazeti nakutana na neno la “Tunaadhimisha miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika kwa Amani,” Kuna wasanii ambao wamediriki kuhimiza na kusifia vitu ambavyo kwao bado ni sitofahamu, lakini kwa upande wa wasanii wa filamu wao bado hawajasema kauli mbiu yao kuhusu kusherehekea miaka 50 ya Uhuru Tanganyika.Ni kweli sote tunataka Amani lakini kuna wakati hata neno hilo linatumika vibaya kwa kuwanufaisha wachache tu, katika tasnia ya filamu toka ilipoingia kama biashara rasmi kwa filamu kuuzwa kama ilivyokuwa kwa kanda za muziki mwaka 2003 kwa filamu ya Girlfriend kwa sasa hali si shwari.
Filamu hiyo ikiingia sokoni kwa mara ya kwanza hadi leo hii umiliki bado umebaki kuwa kwa watayarishaji na si kwa msambazaji, lakini filamu zinazotoka kwa sasa ni mali ya wasambazaji kwa maana ya Hakimiliki na si hakishiriki na hata ukiongea na wahusika ambao ni COSOTA ni kitendawili.
Mijadala mingi yenye mitafaruku imekuwa ikijitokeza kila kukicha katika tasnia hii ya filamu, hata makundi yenye kutangaziana vita wao kwa wao, kuhusu maslahi yao huku ikisemekana kuwa msambazaji mmoja kuegemea upande mmoja katika kulinda maslahi yake.Jambo ambalo lipo wazi hata kazi ya Chama cha Hakimiliki COSOTA kujikuta nacho kikitumia nguvu nyingi katika kulinda kazi za kampuni moja tu kwa kutoa matangazo katika filamu za kampuni hiyo na kujisahau kuwa Chama hicho kila mwanachama wake ambaye amesajili kazi yake anastahili huduma hiyo.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging