Mwanahija Cheka ‘Bibi Cheka’ Ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 51 ambaye hajulikani sana katika medani ya muziki ameamua kujitosa kuimba muziki wa kizazi kipya na amerekodi wimbo uitwao ‘Ni Wewe’.Meneja wa TMK Wanaume Family, Saidi Fella ‘Mkubwa Fella’, aliweka wazi kuwa katika wimbo huo uliorekodiwa studio ya Poteza Records amemshirikisha kinara wa kundi la TMK Wanaume Family Amani Temba ‘Mh Temba’.
Mkubwa Fella alisema kuwa licha ya kutojulikana sana kwenye medani ya muziki lakini uwezo wa Bibi Cheka katika kuimba na kurap ni mkubwa.“Mkubwa! Huyu mama watu wengi hawamjui lakini mimi nasema huyu ni mwanamuziki, alikosa nafasi tu ya kudhihirisha uwezo wake,” alisema Mkubwa Fella.
Picha kwa hisani ya Millard Ayo