Wakati mwanamuziki Charles baba wa Mashujaa Band,Alishikiliwa na Jeshi la Police mara baada ya Aliyekuwa mwajiri wake African Stars,Twanga pepeta,kudai kuwa mwanaamuziki huyo kabla hajaama katika band hiyo alikuwa akidaiwa sh millioni mbili za Kitanzania,mara baada ya hayo kuisha sasa mambo yamehamia Extra Bongo,
Kiongozi wa Bendi hiyo Ally Choki, amesema waimbaji wake wapya EDO BOKASA na FRANK ALMAS kukamatwa na kushikiliwa na polisi kwenye kituo cha Mwananyamala kwa tuhuma za kutoroka na deni la milioni mbili kutoka kwenye bendi waliyokua wakifanya nayo kazi zamani ya TOT.alisikika akisema “ni kweli walikamatwa na sababu kubwa ni hilo deni, lakini nilikwenda na wakapata dhamana na wakakubaliana kwamba deni hilo watakua wanalipunguza kila mwezi na sio wanamuziki wa bendi yangu peke yake, kuna waliokwenda mashujaa na mapacha watatu nao pia wako kwenye hiyo list ya wanaodaiwa”Wanamuziki hao wako nje kwa sasa baada ya kukubaliana kulilipa kidogo kidogo hilo deni...