CMB Prezzo ambaye kwa sasa anatamba na ngoma yake "For sure for shizzle, ameamua kuzungumzia Beef yake na Mwanamuziki ambaye na yeye anaendelea kuingiza mshiko kupitia ngoma yake inayokwenda kwa jina la KIGEUGEU Anajulikana kama Jaguar.kuhusina na swala zima la kupatanishwa ili kumaliza Tofauti zao , Prezzo amesema “nina bonge la saa ila sina time ya kuongea nae kwa sababu hana Adabu, yani hata KOFI ANNAN aje kutupatanisha, SITOKUBALI”
Chanzo cha beef yao kilitokana na kauli nzito za JAGUAR zaidi ya mwaka mmoja uliopita, ambazo amekua akiziendeleza kwamba PREZZO aache kujisifia kila siku kwenye media kuhusu kutupia bling bling, afanye muziki.kinachomkasirisha zaidi PREZZO ni kwamba, alieianza hiyo BEEF ni JAGUAR, na aliianza pasipo kuchokozwa na CMB, na wala haikuwa kutokea Prezzo akamkosea chochote JAGUAR hata kumsema vibaya.
HABARI HII NI KWA HISANI YA AMPLIFIER NA MILLARD AYO