Mwanamuziki mkongwe, mwenye heshima kubwa barani Afrika, Youssou N’dour, ametosa ulaji wa ubalozi wa watoto wa Shirika la Watoto la Umoja wa Mataifa ili apate nafasi ya kugombea uraisN’dour ambaye amekuwa balozi wa Unicef kwa miaka mingi, amelazimika kuachana na kazi hiyo ili aweze kujikita kwenye mbio za kuwania Urais wa Senegal.Kwa mujibu wa taratibu za Unicef, haitakiwi kwa mwanasiasa yeyote kufanya kazi za kibalozi chini ya mwavuli wa shirika hilo.
Vilevile, kwa mtu ambaye ni balozi wa Unicef, pindi anapotaka kujihusisha na siasa, sheria zipo wazi kwamba ni lazima ajiuzulu wadhifa huo wa kijamii.Kutokana na sheria hiyo, N’dour amekubalia kuachia ulaji huo wa ubalozi na kushika siasa kwa maelezo kwamba anataka kufanya kazi kubwa ya kuwakomboa Wasenegal.Kazi ya mwisho aliyoifanya N’Dour chini ya Unicef, ilikuwa Septemba 2011 alipokwenda Kambi ya Daabad, Kaskazini ya Kenya ambako alifanya shughuli za kuwasaidia waathirika wa njaa wapatao 435,000 kutoka Somalia.N’dour, alichaguliwa kuwa balozi wa Unicef tangu Aprili 3, 1991, hivyo amefanya kazi za kibalozi kwa zaidi ya miaka 20.Uchaguzi Mkuu nchini Senegal, unatarajiwa kufanyika Februari 26, mwaka huu na N’dour, anatabiriwa kuchuana vikali na rais wa sasa wa nchi hiyo, Abdoulaye Wade...